Skip to toolbar

Forum Replies Created

Viewing 1 post (of 1 total)
  • wagongarts
    Keymaster
    @wagongarts
    #2339 Reply

    DONDOO ZA MKUTANO TAREHE 24/08/2019.

    Blueprint ya serikali ilitumika kushawishi uungwanishaji wa taasisi za COSOTA, BASATA na BODI YA FILAMU. Taarifa hii haikuwa sahihi. Kifungu cha 3.3.8 cha blueprint kinachozungumzia Creative Sector kinatamka wazi kuitaka serikali kugawanya “separate” majukumu ya COSOTA kwa kuunda Copyright Office na kuiachia COSOTA jukumu la Copyright Management Organisation. Huu ndio ushauri wa wataalamu wa serikali ambao wizara inakwenda tofauti nao.

    Waziri Mwakyembe ametamka kwenye hotuba yaje leo kuwa anaisubiri mapendekezo ya sera toka kwa mshauri (University of Dar es salaam). Moja ya maeneo ya msingi katika kuandika sera ya Sanaa ni UTAWALA WA SANAA ambayo ndio hoja ya wizara leo ya kuunganisha BASATA, COSOTA na BODI YA FILAMU NA MICHEZO YA KUIGIZA. Ni wazi kuwa sera ndio muongozo wa utendaji wa Wizara. Ni kwa vipi ameshawishika kuunganisha taasisi hizi bila kusubiri ushauri wa kitaalamu bado sijapata jibu.

    KUUNGANISHA UTAWALA WA SANAA.
    MIRAHABA.

    Ni mara chache sana binadamu hujisikia uchungu na furaha kwa wakati mmoja. Mama anapojifungua husikia uchungu wa kuzaa na furaha ya kupata mtoto. Hivi ndivyo Waziri Mwakyembe alivyotufanya tujisikie leo aliposema kuwa vyombo vya habari km TV na Radio vimeanza kulipa mirahaba. Furaha sababu ni jambo jema lkn huzuni sababu ni jambo hili lililotakiwa kufanywa kwa usimamizi wa serikali toka mwaka 1999 wakati sheria ya Hakimiliki na Shirikishi ilipopitishwa na Bunge.

    Radio na TV binafsi zimekuwa zikihoji kuwa visibughudhiwe sababu vyombo vya serikali km TBC na Radio Tanzania havilipi.

    Je matrilioni ya shilingi toka mwaka 1999 mpaka leo yatalipwa? Sidhani lkn yetu macho.
    WAZO LA KUUNGANISHA UTAWALA WA SANAA.

    Wawasilisha hoja wa Wizara hawakuzungumzia kabisa mgawanyo kimfumo (structure) na wa kimadaraka wa chombo kipya wanachopendekeza. Hawakutaja wanapendekeza zipi zitakuwa kurugenzi? zipi zitakuwa idara? Zitahusiana vipi? Zitahitaji watu wangapi, kutakuwa na bodi au baraza? Uteuzi au kuchaguliwa vitafanyikaje? Watawafikia vp wasanii mikoani?

    Ukweli ni kwamba kwa mtu aliye makini mapendekezo yao yaliacha naswali mengi bila majibu. Mara kadhaa kauli za “msiwe na wasi tutaweka mambo sawa” zilisikika.

    Haya ni matokeo ya kufanya mambo bila tafiti au tathmini.

    Robert M
    M/kiti
    Tava

Viewing 1 post (of 1 total)
Login Lost Password

wagongarts

Profile picture of wagongarts

@wagongarts

active 11 months, 1 week ago